Psalms 34:11-16


11 aNjooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Bwana.
12 bYeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
13 cbasi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.
14 dAache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.

15 eMacho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
16 fUso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu,
ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
Copyright information for SwhNEN